Jaji asimamishwa kazi baada ya kumfunga pingu mtoto aliyesinzia mahakamani

0
85

Jaji wa Mahakama ya Wilaya ya Detroit nchini Marekani, Kenneth King amesimamishwa kazi kwa muda baada ya kumfunga pingu na kumtishia kumfunga jela msichana mwenye umri wa miaka 15 kwa sababu alionekana kusinzia wakati wa ziara ya shule mahakamani.

Jaji huyo amedai hakufurahishwa na kitendo cha msichana huyo anayejulikana kama Eva Goodman na kuongeza kuwa alitaka kumwonesha mwenendo wake unavyotakiwa kuwa anapokuwa mahakamani.

Mama wa binti huyo, Latoreya Till ameviambia vyombo vya habari kuwa familia yake kwa sasa haina mahali pa kudumu pa kuishi na mwanaye alisinzia mahakamani kwa sababu hakupata muda wa kulala vizuri pamoja na uchovu wa kazi.

“Tunalazimika kuhama hama kwa sasa kwa sababu hatuna makazi ya kudumu. Na hivyo, usiku ule tulifika nyumbani kidogo usiku. Na kwa kawaida, anapoenda kazini, huwa anaamka na kupanda miti au kufanya shughuli nyingine za kimwili,” amesema.

Mama huyo ameeleza kuwa binti yake ni mkarimu na hana shida yoyote lakini kwa sasa amepatwa na uoga sana baada ya kufanyiwa tukio hilo kwenye chumba cha mahakama.

Send this to a friend