Familia ya mwigizaji Alain Delon, ambaye aliaga dunia mwishoni mwa juma akiwa na umri wa miaka 88, imekanusha ombi lake la kutaka mbwa wake anyongwe na kuzikwa kando yake kufuatia kifo chake kilichotokea nchini Ufaransa.
Mwigizaji huyo aliyefariki siku ya Jumapili, katika mahojiano na jarida la Paris mwaka 2018, alimuelezea mbwa wake mpendwa wa Ubelgiji aitwaye Loubo kama mbwa wake wa maisha ambaye alimpenda na kumchukulia kama mtoto wake.
“Nimekuwa na mbwa 50 maishani mwangu, lakini nina uhusiano maalum na huyu,” Delon aliliambia jarida hilo na kuongeza, “Ikiwa nitakufa mbele yake, nitamwomba daktari wa mifugo tufe pamoja. Atamlaza mikononi mwangu.”
Kufuatia ukosoaji kutoka kwa vikundi vya ustawi wa wanyama nchini Ufaransa, familia ya Delon imethibitisha kwamba hawakubaliani na matakwa ya kutatanisha ya mwigizaji huyo.