Rais atoa rai maeneo ya Kizimkazi yatumike vizuri kwa manufaa ya kizazi kijacho

0
19

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa rai kwa wakazi wa maeneo ya Kizimkazi kuyatumia vizuri maeneo yao wanayoyamiliki kwa uangalifu na wasiyatoe bila utaratibu ili yaweze kuwa na manufaa kwa vizazi vijavyo.

Ameyasema hayo leo Agosti 24, 2024 wakati akiweka Jiwe la Msingi mradi wa Kasa Salaam-Cave Kizimkazi Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar, ambapo viongozi mbalimbali pamoja na wananchi wameshiriki.

“Msisahau maeneo tukiondoka duniani, maana msije mkauza [maeneo Kizimkazi] mpaka pa kuzikana tukawa tunapatafuta. Hayo maeneo ni muhimu sana, katika mpango mji huu, hakikisheni tuna eneo ambalo Mungu akituhitaji tunakwenda kupelekwa, zile nyumba zetu za mwisho,” ameeleza.

Aidha, ameeleza kuwa Tamasha la Kizimkazi linalofanyika Visiwani Zanzibar ni tamasha la Kitaifa, hivyo litakuwa mikononi mwa Taifa, huku akiwasihi wana-Kizimkazi kutumia fursa hiyo kukua kiuchumi pamoja na kulinda tamaduni za eneo hilo.

Send this to a friend