Rais Samia ampongeza Odinga kwa kudumisha mahusiano mazuri na viongozi wa Afrika

0
18

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inamuunga mkono Waziri Mkuu Mstaafu wa Kenya, Raila Odinga ambaye anawania nafasi ya Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU).

Ameyasema hayo leo wakati akishiriki hafla ya uzinduzi wa kampeni ya kumnadi mgombea huyo Ikulu jijini Nairobi ambapo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Afrika.

Rais Samia ameeleza kuwa Watanzania wanamfahamu Odinga kama mwanamajumui wa Afrika anayeamini katika mtangamano wa Afrika na manufaa yake huku akimueleza Odinga kama kiongozi mwenye busara na mwenye uwezo wa kujenga Umoja wa Afrika.

Halikadhalika, Rais Samia amempongeza Odinga kwa kudumisha mahusiano mazuri na viongozi wa Afrika na wabia.