Rais Samia aikumbusha jamii kutomsahau mtoto wa kiume katika malezi

0
49

Rais Samia Suluhu Hassan amehimiza wazazi na walezi kuhakikisha kuwa watoto wanalelewa katika mazingira ya heshima, amani na upendo ili kuijenga jamii yenye maadili bora.

Akizungumza wakati akishiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur’aan yaliyofanyika jijini Dar es Salaam leo, amesisitiza umuhimu wa kuendeleza familia na maadili ya nchi, akibainisha kuwa familia yenye misingi imara ni msingi wa taifa lenye nguvu.

“Kwa asili, wanawake wana nafasi kubwa katika ulezi wa familia bora. Kwahiyo kumlea mtoto wa kike katika misingi ya kiimani unakuwa unaandaa mwanamke au mama atakayeishi katika misingi hiyo,” ameeleza.

Aidha, Rais Samia ameikumbusha jamii kutomsahau mtoto wa kiume katika malezi na miongozo ya maadili, kwani watoto wote wanapaswa kulelewa kwa usawa ili kuwa na jamii yenye uwiano.

Mbali na hayo, amesisitiza umuhimu wa haki, amani, kuheshimiana, na kustahimiliana kama nguzo za kuimarisha umoja wetu kama taifa akieleza kuwa mashindano hayo yanachangia katika kuimarisha maadili ya kitaifa na kudumisha mshikamano miongoni mwa wananchi wa Tanzania bila kujali tofauti za kidini au kikabila.

Send this to a friend