Tabia 7 unazopaswa kuepuka ili kulinda afya ya meno yako

0
46

Wengi wetu tunajua umuhimu wa kupiga mswaki na kutumia uzi wa meno, lakini je, unajua kuwa tabia kama kutafuna barafu, kutumia meno kama zana, au hata kupiga mswaki kwa nguvu nyingi vinaweza kudhoofisha meno yako polepole?

Haya ni makosa madogo madogo yanayofanywa ambayo huaribifu meno;

  1. Kutafuna vitu vigumu

Kujaribu kufungua vitu kwa meno au kutafuna vitu vigumu kama barafu, penseli, au karanga ngumu kunaweza kusababisha meno kuvunjika au kupasuka.

  1. Kutumia meno kama zana

Kutumia meno kufungua chupa, kuondoa vifuniko, au kukata vitu kunaweza kuongeza hatari ya kuvunjika au kuharibika.

  1. Kunywa vinywaji vyenye sukari nyingi

Soda, juisi za viwandani, na vinywaji vingine vyenye sukari nyingi vinaweza kusababisha kuoza kwa meno kwa kuongeza bakteria wanaoleta asidi.

  1. Kupiga mswaki kwa nguvu

Kupiga mswaki kwa nguvu nyingi au kutumia mswaki wenye bristles ngumu kunaweza kuharibu enamel ya meno na kuathiri fizi.

  1. Kutokuzingatia usafi wa mdomo

Kutopiga mswaki mara mbili kwa siku, kutotumia uzi wa meno (dental floss), au kutoenda kwa daktari wa meno mara kwa mara kunaweza kusababisha matatizo kama vile kuoza kwa meno au magonjwa ya fizi.

  1. Kuvuta sigara au kutafuna tumbaku

Tumbaku inaharibu meno na fizi, na inaweza kuongeza hatari ya saratani ya kinywa.

  1. Kusaga meno (Bruxism)

Kama unasaga au kukaza meno kutokana na msongo wa mawazo, unaweza kuwa unaathiri meno yako bila kujua. Watu wengi husaga meno yao wakati wakiwa wamelala, hali ambayo inaweza kusababisha maumivu ya kichwa, maumivu ya taya (TMJ), na kuharibika kwa sehemu za kutafunia. Bruxism pia inaweza kusababisha mmomonyoko wa enamel ya meno na kuyafanya meno kuwa na hisia kali zaidi kwa vyakula na vinywaji vya moto na baridi.

  1. Kukata kucha kwa meno

Kukata kucha kwa meno mara nyingi hutokana na msongo wa mawazo, na kawaida huanza utotoni. Mbali na kukuweka kwenye hatari ya kupata vijidudu, tabia hii inaweza kuharibu meno yako kwa muda mrefu. Kama vile kula peremende ngumu na barafu, kukata kucha kunaweza kusababisha kuvunjika kwa meno na katika hali mbaya, unaweza kuathiri misuli ya taya na viungo vya taya.

 

 

Send this to a friend