Serikali kufuatilia utendaji wa watumishi wa afya kwa wagonjwa

0
30

Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema Serikali itaendelea kuhakikisha wauguzi, madaktari na watumishi wote wa Sekta ya Afya wanapata stahiki zao pamoja na kuwasimamia na kufuatilia wajibu wao katika kutekeleza majukumu yao ikiwemo kuwa na lugha zenye staha kwa wagonjwa.

Ameyasema hayo leo wakati akiongea na watumishi pamoja na wagonjwa akiwa kwenye ziara yake ya kukagua huduma zinazotolewa katika Taasisi ya Moyo ya Jakawa Kikwete (JKCI) Jijini Dar Es Salaam.

“Afya ni usalama wa nchi, afya ni maendeleo ya nchi, afya ni jambo la msingi sana katika ustawi wa Taifa, tunasema leo tumefikia uchumi wa kati ni kwa sababu tumeboresha afya za wananchi kwa hiyo ni lazima tusimamie vizuri maslahi ya watumishi lakini na utendaji wao,” amesema Waziri Mhagama.

Aidha, amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo makubwa katika Sekta ya Afya hasa katika uwekezaji wa rasilimali watu pamoja na vifaa, vifaa tiba katika huduma za ubingwa bobezi.

“Tunamshukuru sana Rais Samia Suluhu Hassan, ndani ya miaka mitatu Serikali imewekeza katika utoaji wa huduma za kibingwa ambapo nchi zaidi ya 20 zinakuja Tanzania kupata huduma hizo ikiwemo nchi ya Ujerumani,” amesema.

Send this to a friend