Mwanafunzi ajichoma kisu baada ya kuhojiwa kuiba fedha kwa jirani

0
6

Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mpakani, Ufunuo Mwamlima (13), mkazi wa Tunduma mkoani Songwe, amejiua kwa kujichoma kisu tumboni baada ya kuhojiwa na wazazi wake kuhusu tuhuma za wizi walizozipokea kutoka kwa majirani.

Ufunuo aliamua kuchukua uamuzi huo baada ya kutuhumiwa kuiba kiasi cha fedha kwenye kibanda chao pamoja na kuhojiwa kuhusu mwenendo wake mbovu katika masomo yake ikiwemo kutohudhuria shuleni.

Baba mkubwa wa marehemu, amesema usiku wa Septemba 10, 2024 baada ya wazazi wake kumhoji kijana wao kuhusu tuhuma hizo, alikiri makosa yake ambapo pia alikiri kuwa na chenji alizoiba na alidaii anakwenda kuzichukua ili awaletee lakini muda mfupi baadaye walisikia kelele kutoka jikoni.

“Baada ya kukiri kuiba fedha hizo, alisema chenji zipo chumbani, alipokuwa anakwenda chumbani, akaingia jikoni kuchukua kisu na kumuaga mdogo wake kwa kumpungia mkono na baadaye akajichoma na kisu tumboni,” amesema Mwamlima.

Amesema baada ya kelele hizo wazazi walipotoka walikuta kijana amejichoma kisu na utumbo uko nje na kuamua kumpeleka hospitali, lakini akafariki dunia wakiwa njiani.

Send this to a friend