Watu waliokulia kwenye umasikini huonesha tabia hizi 6 wanapokuwa watu wazima

0
2

Kuna uhusiano wa kina kati ya malezi yetu na mazoea tunayokuwa nayo tukiwa watu wazima. Kukua katika hali ya umaskini kunaweza kututengeneza kwa kiasi kikubwa na kuacha alama ambazo hudumu maisha yote.

Wengi wanaokulia kwenye hali ngumu ya kifedha hukua na ufahamu wa kipekee kuhusu thamani ya rasilimali, wakijenga ustahimilivu wa kipekee mbele ya changamoto za maisha. Lakini nyuma ya ustahimilivu huu, kuna mifumo ya tabia iliyoundwa na hofu ya kurudia hali zile zile walizozikimbia.

Hizi ni tabia 6 zinazooneshwa na watu waliokulia kwenye umasikini pindi wanapokuwa watu wazima;

1. Wanaelewa thamani ya pesa
Watu waliokulia kwenye hali ya umaskini wanaelewa thamani ya pesa zaidi na pia huwa waangalifu kwenye matumizi. Uelewa huu mara nyingi hutafsiriwa kuwa tabia za uchumi wa matumizi zinazoendelea hadi utu uzima.

2. Wana maadili ya kazi
Kukua maskini mara nyingi kunamaanisha kuanza kufanya kazi katika umri mdogo, na mtu anapopata kazi nzuri mara nyingi huwa na bidi ya kazi wakiamini kwamba hakuna kitu kinachokuja bure, na kwamba ikiwa unataka kitu, unapaswa kukifanyia kazi.

3. Hujisikia hatia wanapofanya matumizi
Hata wanapokuwa na uwezo mzuri kifedha, bado wanaweza kujihisi vibaya wanapofanya matumizi kwenye vitu vya starehe au visivyo vya lazima, kwani wamezoea kipaumbele kuwa kwenye mahitaji ya msingi.

4. Wasiwasi kuhusu usalama wa kifedha
Kunaweza kuwa na hofu ya ndani kuhusu mustakabali wa kifedha, hali inayopelekea kuwa na wasiwasi wa kudumu kuhusu usalama wa kazi, akiba, na maandalizi ya uzeeni.

5. Huthamini vitu vidogo
Pesa inapokosekana, starehe ndogondogo zinaweza kuwa na umuhimu mkubwa. Hii mara nyingi husababisha kuthamini sana mambo madogo maishani. Hivyo watu wazima ambao walikulia kwenye umasikini, wanaelewa kuwa furaha haitokani kila wakati na utajiri wa vitu.

6. Ni wastahimilivu
Maisha yamejaa heka heka, na wale ambao wamepitia umaskini mara nyingi hupata ustahimilivu wa kipekee. Inaweza kuwa ngumu, inaweza kuwa changamoto, lakini pia hujenga tabia. Inakufundisha jinsi ya kuinuka unapoangushwa, na jinsi ya kuendelea kusonga mbele, na hali hiyo huendelea hata pindi unapokuwa mtu mzima.