Muhimbili: Gharama za upandikizaji mimba ni milioni 14

0
72

Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) Dar es Salaam imesema gharama za upandikazi mimba ni Shilingi milioni 14.

Akizungumza na Habari Leo, Mkuu wa Kitengo cha Upandikizaji Mimba  MNH, Dkt. Matilda Ngarina amesema upandikizaji mimbahufanyika kwa makundi na hauwezi kufanyika kwa mtu mmoja mmoja hivyo linahitajika kundi la watu kuanzia watano hadi 10 ili kufanya IVF.

“Wakifika watano mpaka 10 tunawaanzishia mzungumko wa hedhi na kuhakikisha wote wameanza hedhi siku moja, kwahiyo tunawapa dawa za kurekebisha mzunguko wao na kulenga tarehe fulani,” amesema.

Ameongeza kuwa “ baadaye tunaanza zile sindano za kuchochea mayai na hizo sindano tunazichoma kwa wiki mbili kisha ndio tunakwenda kule sasa kwenda kunyonya mayai na kuchanganya na mbengu za kiume.”

Aidha, amesema dawa za kusisimua mayai hazipatikani nchini isipokuwa zinaagizwa kutoka nje na kwa gharama kubwa.

“Kuna shida nyingine kwamba zinasafirishwa katika mfumo wa baridi ni mfumo ambao mtu akizembea tu akakata  ule mnyororo wa ubaridi, mtu anaweza asipate mimba kwa sababu kuna vitu vingi ambavyo vinahesabika kwenye ubora wa dawa,” ameeleza.

Ameongeza kuwa mtu yeyote mwenye umri wa kupata mtoto anaweza kundikizwa mimba isipokuwa kwa wale wenye magonjwa ambayo ni hatari kwa upandikizaji mimba kama vile magonjwa ya mapafu, moyo nakadhalika.

 

Send this to a friend