Naibu Rais wa Kenya, Rigathi Gachagua amekanusha madai kwamba alimtaka Rais William Ruto kumpa KSh 8 bilioni [TZS bilioni 169.7] ili kuachia wadhifa wake akijibu kuwa hana tamaa ya pesa bali kipaumbele chake ni kuwahudumia wananchi.
Madai hayo yanahusiana na hoja ya kumng’oa madarakani Naibu Rais Gachagua, ambayo inatarajiwa kuwasilishwa siku ya Jumanne.
UWT yataka BAWACHA kumwomba radhi Rais Samia kwa kumuita muuaji
“Ikiwa ni pesa nilizotaka, ningenunuliwa na wapinzani wa kisiasa ili kuachana na Rais Ruto, lakini sina pupa. Sina mahitaji mengi; watoto wangu ni watu wazima na mke wangu ni mchungaji [..] Siweki pesa kwanza, Wakenya ndio kipaumbele changu,” ameeleza katika kipindi kimoja cha redio nchini humo.
Gachagua anadaiwa kutaka kulipwa fidia kwa kila kura ambayo Ruto aliipata katika eneo lenye kura nyingi la Mlima Kenya analotoka, katika azma yao ya urais mwaka 2022 ili kuondoka ofisini.