Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amewataka maafisa masuhuli kwenye Halmashauri zote nchini waweke msisitizo wa kutumia mifumo ya kielektroniki katika makusanyo badala la kukusanya kwa fedha taslimu ‘Cash’.
Amesema kwa kufanya hivyo kutasaidia kuongeza mapato katika maeneo yao na kuepuka vishawishi vya kutumia vibaya fedha za umma ambazo zinakusanywa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumza leo kwenye kikao na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam, amesema suala la mapato ni lazima liwekewe msisitizo ili kuwe na matokeo mazuri kwenye halmashauri.
Pia ametoa wito kwa wakurugenzi wa Halmashauri kutumia mapato ya ndani katika kutekeleza miradi ya maendeleo badala ya kusubiri fedha kutoka Serikali kuu pekee.
Dkt. Nchemba aishukuru IMF kwa misaada na mikopo nafuu nchini
“Acheni kutegemea mapato ya Serikali kuu pekee, tunataka kuona mapato ya ndani yanatumika katika kutekeleza miradi ya maendeleo.”
Aidha, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma kufanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu ili mipango na malengo ya Serikali ya kuwahudumia Watanzania yaweze kutimia.
Mbali na hayo, amewataka watumishi wa umma wafanye tathmini ya utekelezaji wa miradi mbalimbali katika maeneo yao kwa kuangalia hatua iliyofikiwa na sehemu iliyobaki ili mpaka kufikia June 2025 miradi hiyo iwe imefikia zaidi ya asilimia 95 ya utekelezaji.