Nchi 10 za Afrika zilizowekeza zaidi kwenye ulinzi mwaka 2024

0
6

Katika mwaka 2024, hali ya usalama barani Afrika imekuwa na changamoto nyingi, ikiwa ni pamoja na migogoro ya ndani, ugaidi, na matatizo mengine ya kikanda.

Kwa sababu hiyo, serikali za Afrika zimekuwa na ulazima wa kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika sekta ya ulinzi na usalama ili kuhakikisha ustawi wa nchi zao.

Kwa mujibu wa ripoti ya Global Firepower, ambayo hupima nguvu ya kijeshi ya nchi 145 duniani, Algeria inashikilia nafasi ya kwanza barani Afrika na ya 22 duniani kwa bajeti ya juu ya ulinzi mwaka 2024.

Matumizi haya ya ulinzi yanahusisha ununuzi wa vifaa vya kisasa vya kijeshi, matengenezo ya vifaa hivyo, pamoja na malipo ya pensheni kwa wanajeshi waliostaafu.

Zifuatazo ni nchi 10 za Kiafrika zilizo na bajeti kubwa zaidi ya ulinzi mnamo 2024 (TZS);

1. Algeria: Trilioni 58.7
2. Morocco: Trilioni 32.9
3. Egypt: Trilioni 25.6
4. Nigeria: Trilioni 10.9
5. Libya: Trilioni 9.2
6. South Africa: Trilioni 7.3
7. Kenya: Trilioni 5.9
8. Tanzania: Trilioni 5.0
9. Botswana: Trilioni 4.5
10. Angola: Trilioni 4.4

Chanzo: Business Insider Africa

Send this to a friend