Waziri aagiza polisi kuwakamata viongozi wanaosimamia ujenzi wa kituo cha afya Geita

0
22

Waziri wa Madini, Anthony Mavunde ameagiza Jeshi la Polisi kuwakamata viongozi wa vijiji na Kata waliokuwa wakisimamia mradi wa ujenzi wa kituo cha afya kilichoko Kata ya Ushirika mkoani Geita ambacho kilitengewa shilingi milioni 500 na kuishi pasipo ujenzi kukamilika.

Waziri Mavunde ameitaka Taasisi ya Kupamba na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanakamilisha taratibu zote za kisheria kwa wote waliohusika katika tuhuma hizo ili waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Mkuu wa Mkoa, fedha hizi zikija ni fedha za umma, wanapojitokeza watu wachache ambao wanafanya kwa maslahi yao binafsi naomba mheshimiwa
Mkuu wa Mkoa muendelee kusimamia kupitia vyombo vyetu vya Ulinzi na usalama, hatua zichukuliwe,” amesema.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Martine Shigela amesema ujenzi wa kituo hicho ulianza muda mrefu, na kwamba kusuasua kwa ujenzi huo kunatokana na baadhi ya viongozi akiwemo Afisa Mtendaji na Kamati yake kutotimiza wajibu wao.

Send this to a friend