Mwalimu wa dini akamatwa kwa tuhuma za kubaka watoto

0
25

Jeshi la Polisi mkoani Kagera limemkamata na kumfikisha mahakamani Haruna Ayubu Rubai (63), Mwalimu wa dini ya Kiislamu na Daktari wa viungo anayemiliki kituo chake cha mazoezi ya viungo Bukoba mjini kwa tuhuma za kubaka watoto.

Mtuhumiwa anadaiwa kutenda kosa hilo Oktoba 19 mwaka huu saa saba mchana katika kituo chake cha mazoezi ya viungo kilichopo Kata ya Miembeni, Tarafa ya Rwamishenye, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, ambapo anatuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 12, mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye pia alikuwa mwanafunzi wake wa madrasa.

Taarifa ya Jeshi la Polisi imesema mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya mkoani Kagera kwa ajili ya kupatiwa matibabu na kwa sasa hali yake inaendelea vizuri.

Aidha, Jeshi la Polisi limeongeza kuwa mnamo Oktoba 22, 2024 majira ya saa nane mchana, Rayana Issack aligundua kuwa watoto wake wawili wamebakwa, na mara ya kufikishwa hospitalini ilithibitika kuwa wameingiliwa sehemu zao za siri ambapo baada ya kuhojiwa walimtaja mtuhumiwa Haruna Rubai kuwa ndiye aliyewabaka.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi limegundua kuwa mtuhumiwa huyo amekuwa akitumia mbinu ya kutoa msaada kwa familia zenye uhitaji kila Jumamosi, ambapo baadhi ya familia hizo huwatuma watoto wao kufuata mahitaji yao ofisini kwake, na ndipo hutumia nafasi hiyo kuwafanyia ukatili huo.

Send this to a friend