Dereva wa basi Mwanza – Morogoro anatumia leseni ya pikipiki; Polisi wamkamata

0
21

Dereva wa basi la abiria lenye namba za usajili T 622 EFG linalofanya safari zake mkoani Mwanza kwenda Morogoro anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Mwanza kwa kukutwa na leseni ya kuendesha pikipiki huku akiwa dereva wa basi la abiria.

Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, DCP Ramadhani ng’azi amesema hayo wakati wa ukaguzi wa magari yanayofanya safari za usiku kutoka Jijini Mwanza kuelekea mikoa mingine, ambapo ukaguzi huo ni mwendelezo wa ukaguzi wa magari yasiyokidhi vigezo na masharti ya kubeba abiria ili kuokoa ajali za barabarani zinazotokea mara kwa mara.

“Huyu Sio dereva wa gari la abiria leseni yake ukomo wake ni kuendesha pikipiki. Na tunaendelea na operesheni ya ukaguzi wa magari yanayofanya safari za usiku na yaliyoanza safari zake za mwanza na Shinyanga na katika operesheni hii jumla ya magari yaliyokaguliwa ni mabasi 53, yaliyoandikiwa faini ni mabasi 15, madereva wasiokidhi vigezo 2,” ameeleza Kamanda.

Kwa upande wa abiria wamelishukuru Jeshi la Polisi kwa kuendelea na ukaguzi wa mabasi hayo na kutoa wito kwa Jeshi la Polisi kuomba ukaguzi huo usiwe mwanzo wa safari tu bali hata mwisho wa safari kwani itasaidia kuokoa Maisha ya abiria.

Send this to a friend