Tanzania yashika namba 9 nchi 10 za Afrika zenye miundombinu bora ya barabara

0
72

Miundombinu bora ya barabara ni msingi muhimu kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kuwa inawezesha harakati za watu, bidhaa, na huduma kwa urahisi na ufanisi zaidi na kuchochea ukuaji wa biashara, uzalishaji wa viwanda, kilimo, na sekta nyingine kwa ujumla.

Wakati nchi nyingine za Afrika zimepiga hatua kubwa katika kuendeleza na kutunza miundombinu yao ya barabara, nchi zingine bado zinakabiliwa na changamoto za miundombinu isiyotosheleza, utaratibu duni wa matengenezo, na ukosefu wa uwekezaji katika mifumo ya usafiri.

Kulingana na ripoti iliyopewa jina ‘Cross-Border Road Corridors Expanding Market Access in Africa and Nurturing Continental Integration’, kuna ongezeko la gharama za uzalishaji zinazotokana na ukosefu mkubwa wa miundombinu ya barabara barani Afrika, hali inayochangia matatizo kama vile ucheleweshaji wa usafirishaji, gharama kubwa za matengenezo ya magari, na ukosefu wa upatikanaji wa masoko nakadhalika.

Hii ni orodha ya nchi 10 bora za Afrika zenye miundombinu bora ya barabara mnamo mwaka wa 2024;

1. Namibia
2. Misri
3. Benin
4. Rwanda
5. Mauritius
6. Côte d’Ivoire
7. Morocco
8. Kenya
9. Tanzania
10. Afrika Kusini

Send this to a friend