Ashitakiwa kwa kughushi wosia

0
23

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam imempandisha kizimbani Mohamed Omary (64) mkazi wa Kawe Mzimuni kwa mashitaka mawili ikiwemo kughushi wosia.

Akisoma mashtaka hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Neema Moshi amedai kati ya Julai 29, 1997 na Oktoba 28, 1998 mshtakiwa huyo alighushi wosia wa marehemu Rukia Ahmed maarufu Rukia Sheikh Ali na kuwasilisha wosia huo katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ashikiliwa kwa kudaiwa kumuua rafiki yake kisa wivu wa mapenzi

Wosia huo ulionesha kuwa marehemu ametoa nyumba yake namba 35 kitalu 53 iliyopo Kariakoo kwa Nargi Ahmed Omary, na nyumba namba 60 kitalu M iliyopo Magomeni kwa Mohamed Ahmed Omary wakati akijua kuwa si kweli.

Mshitakiwa huyo amekana mashtaka hayo na kuachiwa huru kwa dhamana, huku kesi hiyo ikiahirishwa hadi Desemba 04, mwaka huu.

Send this to a friend