Baba amuua mtoto wake baada ya kugombana na mke wake

0
48

Polisi katika eneo la Adungosi, Kaunti ya Busia, eneo bunge la Teso Kusini nchini Kenya, wamemkamata mwanamume mwenye umri wa miaka 30 raia wa Uganda kwa kumkata na kumuua binti yake mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu.

Kulingana na taarifa za wenyeji wa eneo hilo, mshukiwa ambaye alikuwa mfugaji wa eneo hilo, alikasirika baada ya kutofautiana na mke wake, ambaye aliripotiwa kuondoka nyumbani baada ya ugomvi huo.

Inaelezwa kuwa baada ya kitendo hicho, mshukiwa anadaiwa kuelekeza hasira zake kwa mtoto wake asiye na hatia, akitumia panga kumshambulia na kumuua.

Wakazi wa eneo hilo walimshambulia kwa ghadhabu mshukiwa kufuatia kitendo chake, lakini alikolewa na polisi waliowasili kwenye eneo la tukio na kuwekwa chini ya ulinzi akisubiri kufikishwa mahakamani.

Mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Alupe wakati uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.

Send this to a friend