Rais Samia aipa TANROADS zaidi ya bilioni 500 ujenzi wa miundombinu Dar es Salaam

0
10

Katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, ametoa zaidi ya Shilingi Bilioni 500 kwa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya miundombinu mkoani Dar es Salaam.

Licha ya kusimamia matengenezo ya barabara na madaraja, katika kipindi cha miaka mitatu, Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya miradi ya Kimkakati ambayo utekelezaji wake upo kwenye hatua mbalimbali sambamba na kuhakikisha mtandao wa kilomita 619 za barabara zinazosimamiwa na TANROADS zinapitika wakati wote.

Hayo yameelezwa na Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Dar es salaam, Mhandisi John Mkumbo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa miradi ya barabara, madaraja pamoja na vivuko katika mkoa huo.

Ameitaja miradi inayoendelea mkoani humo kuwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka BRT awamu ya pili (Km 20.3) inayohusisha barabara ya Kilwa; barabara ya bandari – Gerezani (Kariakoo), Barabara ya Chang’ombe toka makutano ya barabara ya Nyerere hadi Mgulani; Barabara ya Kawawa toka Magomeni hadi barabara ya Nyerere na barabara ya Sokoine toka Gerezani hadi jengo la Mwalimu Nyerere kwa gharama ya Shilingi Bilioni 260.

Ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka BRT awamu ya tatu (Km 23.3) kutoka katikati ya Jiji hadi Gongolamboto na inahusisha barabara za Azikiwe toka Posta ya Zamani hadi Maktaba; Barabara ya Bibi Titi, Barabara ya Nkurumah na barabara ya Nyerere, pia inahusisha ujenzi wa Barabara ya Uhuru kuunganisha mfumo wa usafiri kutoka kituo kikuu cha Gerezani hadi Gongolamboto kwa kupitia Buguruni kwa gharama ya Bilioni 231.

ujenzi wa miundombinu ya mabasi yaendayo haraka BRT awamu ya nne (Km 30.1) kutoka katikati ya Jiji hadi Tegeta ambapo inahusisha barabara ya Ali Hasan Mwinyi kuanzia Maktaba hadi Tegeta pamoja na Sam Nujoma kutoka Mwenge hadi Ubungo kwa gharama ya Shilingi Bil 429

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Send this to a friend