G20 ni kifupi cha ‘Group of Twenty,’ kundi la kimataifa linalojumuisha mataifa 19 yaliyo na uchumi mkubwa zaidi duniani pamoja na Umoja wa Ulaya. Ilianzishwa mwaka 1999 ili kushughulikia changamoto za kiuchumi za kimataifa, ambapo hukutana kila mwaka katika kilele cha mkutano na kujadili masuala muhimu.
Kabla ya kufanyika kwa mageuzi na kuwa G20 mkutano huu ulijulikana kama G8 ukiwa na wanachama 8 tu; Canada, France, Germany, Italy, Japan, Russia, Ulaya, na Marekani. Marais wa Tanzania wa kipindi cha mwaka 2005, Hayati Benjamin Mkapa na mwaka 2008, Jakaya Kikwete waliwahi kushiriki.
Orodha ya Wakuu wa nchi na Serikali wanawake waliowahi kushiriki Mkutano wa G20;
Cristina Fernández de Kirchner
Huyu ni Rais Mstaafu wa Argentina aliyeshikilia nafasi hiyo kuanzia mwaka 2007 hadi mwaka 2015. Wakati wa uongozi wake ndipo Mkutano wa Viongozi Wakuu wa Nchi wa Kundi la G20 ulioanzishwa mwaka 1999 ulibadilishwa jina kutoka G8 hadi G20 mwaka 2008 na Rais Kircher kushiriki Mkutano wa G20 uliofanyika Pittsburgh, Marekani mwaka 2009.
Julia Gillard
Mkutano wa G20 wa mwaka 2010 ulifanyika jijini Seoul, Jamhuri ya Korea. Waziri Mkuu wa Australia wa kipindi hicho naye alishiriki. Kwa nchi ya Australia, Waziri Mkuu ndio kiongozi wa ngazi ya juu zaidi ya nchi kama ilivyo Rais kwa nchi yetu. Julia Gillard alihudumu kama Waziri Mkuu wa Australia mwaka 2010 hadi 2013. Alishiriki mikutano ya G20 kwa mwaka 2011, 2012, 2013 na 2014.
Dilma Rousseff
Katika kipindi cha mwaka 2011 hadi 2016, Dilma Rousseff alihuduma kama Rais wa Brazil naye kama ilivyokuwa kwa Gillard, katika kipindi cha kwanza cha uongozi wake, aliweza kushiriki katika Mkutano wa G20 wa mwaka huo uliofanyika Ufaransa. Kwa ujumla Rousseff amewahi kushiriki mikutano mitatu ya G20, ikiwemo ya mwaka 2013 nchini Russia na 2014 nchini Australia.
Angela Markel
Mwanasiasa mkongwe na Kansela Mstaafu wa Ujerumani, Angela Markel ndiye kiongozi aliyeweka historia hadi sasa ya kuhudhuria mikutano mingi zaidi ya G20 akiwa madarakani kati ya mwaka 2005 na 2021. kansela Mkuu ndiyo nafasi ya juu zaidi nchini Ujerumani
Samia Suluhu Hassan
Mwaka huu 2024, Rais Samia Suluhu Hassan alipokea mwaliko wa kushiriki Mkutano wa G20 kutoka kwa Rais wa Brazil, Luiz Inácio Lula da Silva. Kushiriki kwake Mkutano huu wa 19 wa G20 kunamfanya Rais Samia Suluhu kuwa Rais wa kwanza mwanamke wa Afrika kualikwa kushiriki katika mkutano wa G20 na Rais wa kwanza wa Tanzania kushiriki Mkutano wa G20.
Kaulimbiu ya Mkutano wa Mwaka huu inasema Building a Just World and a Sustainable Planet, yaani Kujenga jamii yenye haki, usawa na Maendeleo Endelevu huku ajenda kuu za mkutano wa G20 Brasil ni katika kupambana na umaskini, njaa, mageuzi katika nishati na utunzaji wa mazingira.
Claudia Sheinbaum Pardo
Huyu ni Rais wa Mexico ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2018 hadi sasa. Katika Mkutano wa mwaka huu wa G20 Brasil, Rais Samia si Rais mwanamke pekee kwani Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum Pardo naye ameshiriki katika mkutano huu. Kwa mara ya kwanza Rais Pardo alishiriki mkutano huu akiwa Meya wa jiji la Mexico.