Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza kuchunguzwa kwa taarifa ya wanafunzi 14 wa Shule ya Msingi Izinga, iliyopo Nkasi Kusini, Rukwa kufukuzwa shule kwa madai ya wazazi wao kuiunga mkono Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Agizo hilo limekuja baada ya taarifa hiyo kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, ambapo Waziri Mkenda ameielekeza timu ya wataalamu Udhibiti Ubora kwenda kuchunguza ukweli wa taarifa hiyo.
“Nimeona taarifa za wanafunzi kwamba waliondolewa shule kwasababu wazazi wao ni wanachama wa CHADEMA, nimeshangazwa sana na taarifa hii, na tayari timu yetu ya wadhibiti ubora nimeituma asubuhi hii ifike pale shuleni ituambie ukweli kuhusu jambo hili.
Rais Samia kuunda Tume kushughulikia suala la Ngorongoro
Aidha, Profesa Mkenda amesema watoto wote wa Kitanzania wana haki ya kusoma, hivyo hakuna mwenye mamlaka ya kumtoa mtoto shuleni kwa sababu za vyama.
Chanzo: Mwananchi