Kufuatia taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inayodai Askari Polisi kuvamia ofisi za Taasisi ya Reach Out Tanzania iliyopo eneo la Makumbusho kwa lengo la kumkamata Mwanasheria wa taasisi hiyo, Alphonce Lusako, Jeshi la Polisi limesema askari hao walifika kumkamata mtuhumiwa aliyetajwa kwa jina la Emmanuel Mweta na si Mwanasheria huyo kama inavyoelezwa.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema kuwa askari walifika eneo hilo kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye hapo awali alikamatwa, na baada ya kudhaminiwa aliruka dhamana kwa muda mrefu.
Polisi wamesema walipokea taarifa leo Desemba 05, 2024 kutoka kwa mlalamikaji kuwa amemwona mtuhumiwa huyo, hivyo ikabidi wawahi haraka kumkamata.
Serikali: Tunachunguza madai ya wanafunzi kufukuzwa kisa wazazi wao wanaunga mkono CHADEMA
“Tunaendelea na uchunguzi kubaini ni nini kilichomfanya anayetajwa kwa jina la Alphonce Lusako kukimbia kisha kujirekodi na kuirusha kwenye mitandao wakati siyo yeye aliyekuwa anatafutwa na Askari waliofika pale.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa Askari hao waliovalia mavazi ya kiraia walijitambulisha kwake na kumweleza kuwa wamefika pale kwa nia ya kumtafuta Emmanuel Mweta.