Waziri Kuu: Tumedhamiria kuendelea kutatua changamoto za walimu

0
16

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendelea kutatua changamoto za walimu zikiwemo za malimbikizo ya madeni na upandishaji wa madaraja.

Amesema hayo alipomwakilisha Rais Samia Suluhu katika mkutano wa 19 wa Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari (TAHOSSA) jijini Dodoma ambapo amesema Rais Samia anatambua, anathamini na kuheshimu kazi kubwa inayofanywa na walimu wote nchini katika kuhakikisha wanashiriki kikamilifu kukuza na kuiendeleza sekta ya elimu nchini.

“Kwa sasa suala la stahiki za walimu linaendelea kuzingatiwa, na Serikali imeendelea kufanya jitihada kubwa za kuhakikisha inapadisha madaraja watumishi walimu waliokosa na wanaopaswa kupandishwa, Serikali imedhamiria kuondoa msamiati wa areas (malimbikizo ya mishahara),” amesema.

Ameongeza kuwa katika kipindi cha mwaka 2021/2022 hadi mwaka 2023/2024, Serikali imepandisha madaraja ya walimu 227,383 na kuwabadilishia miundo walimu 20,436

Aidha, Waziri Mkuu amesema katika kipindi cha 2021/22 hadi 2023/24, jumla ya shilingi trilioni 1.76 zimetolewa na Serikali kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya shule ikiwemo ukarabati na ujenzi mpya.

Send this to a friend