Wanafunzi watano wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) wamekamatwa kwa makosa ya wizi wa zaidi ya Shilingi milioni 20 kwa njia ya mtandao.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, Almachusi Mchunguzi amethibitisha kukamatwa kwa wanafunzi hao akiwataja kuwa ni Peter Babuya, Said Amiri (20), Athuman Amiri (24), Brayan Mayunga , Festio Madenge (26) (si mwanafunzi) ambaye yeye ni wakala na James Nathaniel (24).
Jeshi la Polisi limesema watuhumiwa hao wote walikamatwa kwa nyakati tofauti katika maeneo mbalimbali baada ya kujifanya mawakala wa kujitegemea wa kampuni mbalimbali za mitandao na kuiba fedha hizo.
Kamanda MchunguI amesema watuhumiwa hao walioiba fedha hizo mali ya mfanyabiashara na mkazi wa Wilaya ya Muheza mkoani humo, Abdul Shedafa ambapo wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani kusomewa mashitaka yao.