Bwana harusi aliyejiteka apandishwa mahakamani

0
38

Vincent Masawe (36) mkazi wa Kigamboni na Bwana harusi aliyepotea katika mazingira ya kutatanisha na baadaye kupatikana akiwa kwa amejificha kwa mganga wa kienyeji Chakechake Kisiwani Pemba amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na tuhuma za wizi wa gari na fedha.

Wakili wa Serikali, Frank Lomuli amesema Masawe anatuhumiwa kwa wizi wa gari aina ya Ractis yenye thamani ya TZS milioni 15 mali ya Sylvester Masawe ambalo aliliazima ili kulitumia katika shughuli ya harusi kisha gari hilo aliliuza. Na kosa la pili ni kuiba fedha kiasi cha shilingi milioni tatu ambapo alichukua fedha hizo na kuahidi atazirudisha lakini hakufanya hivyo.

Baada ya kusomewa mashtaka hayo, mtuhumiwa alikana mashtaka yote, na kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 07, 2025. Mtuhumiwa yuko nje kwa dhamana.

Send this to a friend