Akubali kutalakiana na mume wake kuliko kurudi kijijini

0
18

Mdaiwa Tumaini Angumbwike (35) mkazi wa Makunguru ameiambia Mahakama ya Mwanzo mkoani Mbeya kuwa yuko tayari kutalakiana na mume wake kuliko kurudi kijijini.

Angumbwike ameiambia mahakama kuwa migogoro inayoendelea kati yake na mume wake, ilianza baada ya maisha yao kuwa magumu kutokana na biashara yake kuyumba, hivyo mume wake kumtaka warudi kijijini kuanza maisha mapya.

“Maisha niliyoyaishi kipindi hicho kijijini tena nirudi kuyaishi, hapana. Ndio maana nilitafuta mwanaume mjini kuondokana na maisha ya kijijini,” ameeleza.

Ameongeza kuwa “ Mheshimiwa Hakimu, huyu mwanaume nampenda sana na migogoro iliyopo kati yetu ni mimi kugoma kurudi kijijini, hivyo nilimruhusu yeye arudi kijijini akajipange na mimi kuniacha mjini, lakini cha ajabu aliporejea kijijini alitafuta mke mwingine.”

Hapo awali mdai katika kesi hiyo aliomba kuvunja ndoa hiyo kwa madai kuwa wametengana kwa zaidi ya miaka minne pasipo mke wake kumpa huduma muhimu ikiwemo tendo la ndoa.

Kesi hiyo imeahirishwa mpaka Januari 07, mwaka huu.

Send this to a friend