Nchi 10 za Afrika zinazoongoza katika uwekezaji wa sekta binafsi

0
17

Benki ya Dunia imeripoti kuwa Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara inapaswa kuwekeza takriban asilimia 7.1 ya Pato la Taifa (GDP) kila mwaka ili kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu, huku kiwango cha sasa cha uwekezaji kikiwa ni asilimia 3.5 pekee ya GDP.

Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) inakadiria kuwa bara hili linahitaji kati ya dola bilioni 130 hadi 170 kila mwaka ili kukidhi mahitaji ya miundombinu. Hata hivyo, pengo la ufadhili bado ni kubwa, likifikia upungufu wa dola bilioni 100 kila mwaka.

Serikali pekee haziwezi kubeba mzigo huu wa kifedha, na hivyo mtaji wa kutoka sekta binafsi umekuwa sehemu muhimu ya suluhisho. Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC), mwanachama wa Kikundi cha Benki ya Dunia, limekuwa na jukumu muhimu katika kuhamasisha uwekezaji wa sekta binafsi barani Afrika.

Kwa kufadhili miradi ya miundombinu na kushauri serikali jinsi ya kuunda ushirikiano wa sekta ya umma na binafsi (PPPs), IFC inaunda mazingira yanayovutia mtaji wa kibinafsi kustawi. Katika mwaka wa fedha wa 2024 (FY24), IFC ilihamasisha ufadhili wa dola bilioni 22.5, ongezeko la asilimia 50 ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2023 (FY23).

Hizi ni nchi 10 za Afrika zinazoongoza katika uwekezaji wa sekta binafsi kwa hisani ya Benki ya Dunia (TZS);

1. Afrika Kusini: Trilioni 12.5
2. Nigeria: Trilioni 9.7
3. Misri: Trilioni 8.2
4. Ethiopia: Trilioni 5.6
5. Cote D’Ivoire: Trilioni 5.3
6. Kenya: Trilioni 4.1
7. Guinea: Trilioni 3.6
8. Msumbiji: Trilioni 3.2
9. Morocco: Trilioni 2.1
10. Cameroon: Trilioni 1.9

Chanzo: Business Insider Africa

Send this to a friend