Sababu za CAF kuahirisha mashindano ya CHAN hadi Agosti 2025

0
16

Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) leo limetangaza kuahirisha Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies CAF (CHAN) Kenya, Tanzania, Uganda 2024 hadi Agosti 2025.

Hatua hiyo imefuata baada ya wataalam wa Kiufundi na Miundombinu wa CAF ambao baadhi yao wameweka kambi nchini Kenya, Tanzania, na Uganda, kuishauri CAF kuwa muda zaidi unahitajika ili kuhakikisha miundombinu na vifaa vinakidhi viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kuandaa Mashindano hayo.

Rais wa CAF, Dk. Patrice Motsepe amesema “Ningependa kutoa shukrani za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania, na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea, na maendeleo mazuri yaliyofikiwa katika ujenzi na ukarabati wa viwanja vya michezo, viwanja vya mazoezi, hoteli, hospitali, pamoja na miundombinu na vifaa vingine nchini Kenya, Tanzania, na Uganda kwa ajili ya kuandaa Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies CAF (CHAN) Kenya, Tanzania, Uganda 2024 kwa mafanikio.

Nina uhakika kuwa viwanja, viwanja vya mazoezi, hoteli, hospitali, pamoja na miundombinu na vifaa vingine vitafikia viwango vinavyohitajika na CAF kwa ajili ya kuandaa Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies CAF (CHAN) Kenya, Tanzania, Uganda 2024 kwa mafanikio mnamo Agosti 2025.”

CAF itafanya Droo ya Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies CAF (CHAN) Kenya, Tanzania, Uganda 2024 nchini Nairobi siku ya Jumatano, Januari 15, 2025

CAF amesema tarehe kamili ya kuanza kwa Mashindano ya Mataifa ya Afrika ya TotalEnergies CAF (CHAN) Kenya, Tanzania, Uganda 2024 mnamo Agosti 2025 itatangazwa kwa wakati muafaka.

Send this to a friend