Watoto wawili walioibiwa wapatikana kwa mganga wa kienyeji, dada wa kazi ahusishwa
Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwapata watoto wawili wakiume na wakike nyumbani kwa mganga wa kienyeji anayefahamika kwa jina la Abdulikarim mkazi wa Kimara baruti.
Akizungumza na waandishi wa Habari Leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda Jeshi la Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam, SACP Jumanne Muliro amesema watoto hao wamefanyiwa vipimo na kukutwa Afya zao zikiwa njema na tayari wamekabidhiwa kwa wazazi wao.
“January 12,2025 tulipata taarifa za kuibwa watoto wawili wadogo mmoja wa kike mingine wakiume, mmoja miaka mitano mwingine minne, dada wa kazi kwa kushirikiana na mganga wa kienyeji Kimara walishirikiana kufanya kitendo cha kihalifu kuiba Watoto,” amesema SACP Jumanne Muliro
Aidha, amesema watuhumiwa hao wanasubiri kufikishwa Mahakamani baada ya uchunguzi kukamilika.