Nchi 10 za Afrika zenye deni kubwa IMF mwanzoni mwa mwaka 2025
Mikopo ya IMF inaweza kutoa msaada mkubwa wakati wa mdororo wa kiuchumi, lakini kuanza mwaka mpya na deni kubwa kwa IMF, huleta changamoto kubwa kwani inaweza kudhoofisha uchumi, kukwamisha juhudi za maendeleo, na kuhatarisha uhuru wa kitaifa, na hivyo kuziacha serikali zikiwa na nafasi ndogo ya kukidhi mahitaji yao ya haraka.
Nchi nyingi za Afrika zinatarajiwa kuwa na pato kubwa la kiuchumi mwaka 2025, jambo ambalo litazifanya zisiweze kuhitaji mikopo zaidi. Hata hivyo, baadhi ya nchi hizi zimekusanya madeni makubwa katika miaka ya hivi karibuni, jambo ambalo linaweza kuzuia ugawaji sahihi wa fedha za serikali.
Mikopo ya IMF mara nyingi huambatana na masharti magumu, kama vile hatua za kubana matumizi ili kuhakikisha urejeshaji wa deni. Masharti haya mara nyingi hulazimisha mataifa kupunguza matumizi ya umma, kuongeza kodi, au kubadilisha ruzuku.
Deni la nje la Afrika limeongezeka sana katika muongo uliopita, likifikia kiwango cha juu cha dola bilioni 656 mnamo mwaka 2022.
Hii ilitokana na kupungua kwa mapato ya mauzo ya nje na ukuaji wa uchumi wa polepole. Kwa mfano, kiwango cha ukuaji wa Afrika mwaka 2022 kilikadiriwa kuwa asilimia 3.5, lakini bado kilikuwa chini ya wastani wa kabla ya janga la COVID-19 wa asilimia 4.5.
Hizi ni nchi 10 za Afrika zenye deni kubwa zaidi kwa IMF mwanzoni mwa mwaka 2025 kwa mujibu wa ripoti ya IMF;
1. Misri: Trilioni 21.9
2. Kenya: Trilioni 7.6
3. Angola: Trilioni 7.3
4. Cote d’Ivoire: Trilioni 6.9
5. Ghana: Trilioni 6.3
6. DR Congo: Trilioni 4.5
7. Ethiopia: Trilioni 3.3
8. Afrika Kusini: Trilioni 2.8
9. Cameroon: Trilioni 2.78
10. Senegal: Trilioni 2.7
Chanzo: Business Insider Africa