Daraja la Kigongo Busisi kukamilika mwezi ujao

0
13

Serikali imesema ujenzi wa daraja la kimkakati la Kigongo Busisi mkoani Mwanza unatarajiwa kukamilika mwezi ujao, huku likitumia zaidi ya shilingi bilioni 611 hadi sasa.

Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega amesema ujenzi wa daraja hilo umefikia asilimia 96, na endapo mambo yatakwenda kama yalivyo, utafikia asilimia 100 na kukamilika mwezi Februari mwaka huu.

Aidha, Waziri Ulega amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan ambaye wakati anaingia madarakani mwaka 2021 alikuta ujenzi wa daraja hilo ukiwa umefikia asilimia 25 tu.

Daraja hilo linatarajiwa kurahisisha usafiri katika eneo zima la Kanda ya Ziwa kwa kupunguza muda wa usafiri kuvuka kutoka eneo hilo kutoka saa mbili za sasa hadi dakika tano baada ya kukamilika kwa daraja.

Send this to a friend