Nchi zinazoongozwa na jeshi Mali, Niger, na Burkina Faso zimejiondoa rasmi katika Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS).
Nchi hizo ziliunda muungano wake unaojulikana kama Alliance of Sahel States (AES), baada ya ECOWAS kushutumu mapinduzi ya kijeshi na kusimamisha ushirika wao, kwa matumaini ya kurejesha utawala wa demokrasia.
Maelfu ya watu walikusanyika katika nchi za Niger, Burkina Faso na Mali siku ya Jumanne kuunga mkono kujiondoa kutoka kwa muungano wa eneo ambako kunaanza rasmi Jumatano.
Nchi hizo tatu zilikosoa ECOWAS kwa vikwazo ilivyowawekea baada ya mapinduzi na sasa zinapanga kuunda jeshi la umoja na kukuza uchumi kupitia muungano mpya wa maeneo ya Sahel.