Madereva wa malori kutoka Tanzania wakwama DRC kufuatia machafuko

0
7

Madereva kadhaa wa malori kutoka Tanzania wamekwama katika mji wa Goma, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), kutokana na machafuko yanayoendelea katika eneo hilo.

Chama cha Wafanyakazi wa Madereva wa Malori Tanzania (CHAWAMATA) kimethibitisha kuwa ubalozi wa Tanzania nchini DRC unashughulikia kwa karibu hali hiyo ili kuhakikisha usalama wa madereva hao.

“Tangu tulipopata taarifa za hali hii, tumekuwa tukiwasiliana mara kwa mara na ubalozi wetu na wametuhakikishia kuwa Watanzania wote, wakiwemo madereva wetu, watapatiwa msaada wanaohitaji. Tunaona video mtandaoni zikionyesha madereva wakihitaji msaada, jambo linalodhihirisha kuwa hali bado ni mbaya,” amesema Mwenyekiti wa CHAWAMATA, Nuhu Mgodoka alipokuwa akizungumza na Mwananchi.

Kwa sasa, madereva 43 wamethibitishwa kukwama Goma, ingawa idadi hiyo huenda ikazidi 50, kwani wengine wanaripotiwa kuwa katika maeneo mengine kama Jambo Safari.

Serikali ya Tanzania imesema inafuatilia kwa karibu hali hiyo kwa kushirikiana na ubalozi wake nchini DRC ili kuhakikisha usalama wa madereva hao.

 

 

Send this to a friend