Rais Tshisekedi kutohudhuria majadiliano ya EAC kuhusu mgogoro na Rwanda

0
4

Rais wa DRC, Félix Tshisekedi amesema hatashiriki mkutano wa dharura wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ulioitishwa na Rais wa Kenya, William Ruto kuhusu mgogoro wa kiusalama mashariki mwa jimbo la Kivu kaskazini.

Rais Ruto alisema kuwa amezungumza na Rais Tshisekedi na Rais wa Rwanda, Paul Kagame ili kujaribu kutuliza hali inayoendelea katika eneo hilo.

Hata hivyo, msemaji wa Rais Kagame amethibitisha kuwa kiongozi huyo wa Rwanda atahudhuria mkutano huo uliopangwa kufanyika leo.

Wakati huo huo, waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda wameingia katika mji wa Goma, hali ambayo imezua wasiwasi mkubwa. Waangalizi wa kimataifa, ikiwa ni pamoja na Umoja wa Mataifa, Marekani, China, na Umoja wa Ulaya, wameitaka Rwanda kuondoa vikosi vyake kutoka eneo hilo.

Katika mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliofanyika Jumanne, DRC ilitoa wito kwa nchi wanachama kuwa na ujasiri wa kufanya kile kilicho sahihi.

 

Send this to a friend