Nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU

0
40

Mapema wiki hii, Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilitangaza kusitisha kwa muda wa siku 90 utoaji wa fedha kutoka kwa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na UKIMWI (PEPFAR). Mpango huo umekuwa msaada mkubwa katika kutoa matibabu ya VVU barani Afrika na katika mataifa mengine yanayoendelea.

Katika juhudi za kuhakikisha huduma za matibabu hazikatizwi, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, alitangaza kuidhinishwa kwa “Msamaha wa Dharura wa Kibinadamu”, ambao utahakikisha upatikanaji wa matibabu ya VVU yanayofadhiliwa na Marekani hausimamishwi.

Kwa mujibu wa tamko hilo, misaada hiyo itajumuisha dawa muhimu, huduma za matibabu, chakula, makazi, na mahitaji mengine ya msingi yanayohitajika kwa waathirika wa VVU.

Nchi 10 za Afrika zenye kiwango cha juu cha ukosefu wa ajira

Kwa mujibu wa Statista, Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara linaendelea kuwa kitovu cha maambukizi ya VVU duniani, huku mamilioni ya watu wakiishi na virusi hivyo na maelfu zaidi wakiambukizwa kila mwaka. Afrika Kusini inaongoza kwa idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU barani Afrika.

Hizi ni nchi 10 za Afrika zenye idadi kubwa ya watu wanaoishi na VVU;

1. Afrika Kusini: 7,700,000
2. Msumbiji: 2,400,000
3. Nigeria: 1,700,000
4. Uganda: 1,500,000
5. Kenya: 1,400,000
6. Zambia: 1,300,000
7. Zimbabwe: 1,300,000
8. Malawi: 980,000
9. Ethiopia: 610,000
10. DRC: 520,000

Chanzo: Business Insider Africa

Send this to a friend