Trump atangaza kusitisha misaada Afrika Kusini

0
2

Rais wa Marekani, Donald Trump, amedai kuwa Afrika Kusini inataifisha ardhi na kuwatendea vibaya watu wa tabaka fulani, kutokana na hayo, ametangaza kusitisha kutoa misaada kwa nchi hiyo hadi uchunguzi utakapofanyika.

“Marekani haitasimama kwa hilo, tutachukua hatua. Pia, nitakata ufadhili wote ujao kwa Afrika Kusini hadi uchunguzi kamili wa hali hii utakapokamilika

Haijulikani ni nini kilisababisha Rais Trump kuutuma ujumbe huo, Ubalozi wa Afrika Kusini nchini Marekani pia haujatoa maoni kuhusu ujumbe huo.

Mwezi uliopita, Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa alisema hana wasiwasi kuhusu uhusiano wa nchi hiyo na Trump, akisema alizungumza na Trump baada ya ushindi wa uchaguzi na anatazamia kufanya kazi na utawala wake.

Mwaka 2023, Marekani ilitoa karibu Dola milioni 440 kwa ajili ya misaada kwa Afrika Kusini.

 

 

Send this to a friend