Rais Kagame asema hajui kama wanajeshi wa Rwanda wako DRC

0
0

Rais wa Rwanda, Paul Kagame amesema hafahamu kama wanajeshi wa nchi yake wako mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), ambako mapigano kati ya kundi la waasi la M23 na wanajeshi wa Congo yanaendelea.

Sehemu kubwa ya Jumuiya ya Kimataifa inaamini kwamba Rwanda inaunga mkono waasi wa M23, ambao walidai kuuteka mji wa Goma mashariki mwa Congo wiki iliyopita.

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wanaamini kuwa takriban wanajeshi wa Rwanda 3,000 hadi 4,000 wanawasaidia wapiganaji wa M23 mashariki mwa DRC, huku wakiwazidi idadi waasi hao ndani ya nchi hiyo.

“Kuna mambo mengi sijui. Lakini ikiwa unataka kuniuliza, je, kuna tatizo ndani ya Congo linaloihusu Rwanda? Na kwamba Rwanda inaweza kufanya lolote kujilinda? Nitasema kwa asilimia 100,” amesema.

Mapigano yanayoendelea nchini DRC yamesababisha vifo vya zaidi ya watu 700 na kujeruhi maelfu ya watu.