Makamu wa Rais Ufilipino aondolewa madarakani na Bunge kwa kupanga kumuua Rais

0
8

Bunge la Ufilipino limepiga kura ya kumwondoa madarakani Makamu wa Rais, Sara Duterte anayekabiliwa na tuhuma mbalimbali, zikiwemo matumizi mabaya ya fedha za umma na madai ya kupanga njama za kumuua Rais Ferdinand Marcos Jr.

Duterte na Rais Marcos ambao wote wametokea familia mashuhuri kisiasa, waliungana kugombea uchaguzi wa mwaka 2022, lakini muda mfupi baadaye baada ya kushinda uchaguzi, ushirikiano wao ulivunjika.

Trump asema Marekani itaichukua na kuimiliki Gaza baada ya kuwaondoa Wapalestina

Duterte amekanusha madai ya ufisadi na amesema kuwa hatua ya kumuondoa madarakani ni chuki ya kisiasa dhidi yake, huku Marcos akikanusha kuhusika katika mchakato wa kumwondoa madarakani.

Hatima ya Duterte sasa inategemea maseneta 24 wa Ufilipino, ambapo theluthi mbili kati yao wanahitaji kupiga kura kumwondoa madarakani ili kumfungia kushika nafasi za umma katika siku zijazo.

Send this to a friend