Barabara zitakazofungwa katika mkutano wa SADC

0
1

Tanzania imepata fursa ya kuwa mwenyeji wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) ambapo Mkutano huo utakuwa chini ya uenyeji wa Rais Samia Suluhu Hassan.

Kufuatia ugeni huo Jeshi la Polisi limesema hali ya usalama imeimarishwa maradufu Februari 07, hadi 08, 2025 ambapo limetangaza kuwa baadhi ya barabara zitakuwa zinafungwa kwa muda na kufunguliwa haraka kupisha misafara ya viongozi wa Mkutano huo.

Barabara hizo ni;

 

  1. Barabara ya Nyerere kutokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere kwenda katikati ya Jiji.
  2. Barabara ya Sokoine, Kivukoni na Lithuli kuanzia taa za Gerezani kwenda Hoteli ya Johari Rotana, Hyatt Regency hadi Ikulu.
  3. Barabara ya Ohio kutokea Kivukoni kwenda Hoteli ya Serena.
  4. Barabara ya Garden kutokea barabara ya Lithuli kwenda Hoteli ya Southern Sun.
Send this to a friend