![](https://swahilitimes.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/akamatwa-pic-905x613-1.jpg)
Jeshi la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Stephano Maswala (35), mlezi wa kituo cha kulea watoto yatima kilichopo Mlandizi kwa kosa la kubaka watoto watano waishio kituoni hapo kwa nyakati tofauti kuanzia mwezi Oktoba 2024 hadi Januari 2025.
Taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi imesema mtuhumiwa alikuwa akiwabaka watoto hao akiwadanganya kuwa anawatengeneza kisaikolojia ili wasisumbuliwe na wanaume mtaani na waweze kufanya vizuri kwenye masomo ya Sekondari.
Aidha, Jeshi la Polisi limesema taratibu za upelelezi dhidi ya mtuhumiwa huyo zinaendelea na kwa sasa anahojiwa kwa kina kwa kushirikiana na Idara nyingine za Serikali, na mara baada ya kukamilika taratibu hizo atafikishwa mahakamani.