Hamas yaachilia miili ya Waisrael wanne waliokuwa mateka

0
3

Kundi la Hamas limeachilia miili ya watu wanne akiwemo mwanamke na watoto wake wawili, pamoja na mwanaume mzee mwenye umri wa miaka 83, ambao walitekwa wakati wa shambulio la Oktoba 2023.

Miili hiyo imekabidhiwa kwa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu (ICRC) huko Khan Younis, kusini mwa Gaza.

Msemaji wa kundi la Wapalestina amesema wote wanne walikuwa hai kabla ya ndege za kivita za Israel kulenga kwa makusudi maeneo walikokuwa wakiwekwa.

Hamas imesema katika taarifa yake kwamba ililinda maisha ya mateka na kuwapa kile ilichoweza, na iliwatendea ubinadamu, “lakini jeshi lao [Israeli] liliwaua pamoja na watekaji wao.”

Send this to a friend