Meneja kampuni ya LBL Katavi na wenzake watatu wakamatwa kwa kufanya biashara ya upatu mtandaoni

0
5

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linawashikilia watu wanne akiwemo Meneja wa Kampuni ya LBL mkoani humo, Ashery Birutsi (35), Paschal Mathias (34), Ludovick Hussein (35) na Vicent Msita (30) kwa tuhuma za kujihusisha na biashara ya upatu mtandaoni bila kuwa na kibali.

Kupitia taarifa ya Jeshi la Polisi, imesema ilipata taarifa ya uwepo wa kampuni iitwayo Leo Burnett London (LBL) inayojihusisha na biashara ya upatu mtandaoni na ndipo Februari 18, 2025 lilifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao baada ya uchunguzi maeneo ya soko la matunda Manispaa ya Mpanda mkoani humo.

“Katika mahojiano na watuhumiwa hao wameeleza kuwa wamekuwa wakijihusisha na biashara ya upatu mtandaoni na mpaka sasa wameshaunganisha jumla ya wananchi wapatao 85.

Wamekuwa wakituma link maalum kwa wateja ili kujiunga mtandaoni na kisha wateja kutakiwa kulipa fedha kuanzia TZS 50,000 hadi 540,000 na kutakiwa kuangalia matangazo ya video fupi mbalimbali zilizowekwa kwenye mtandao wao kwa madai kwamba watapata faida baada ya kuwekeza fedha zao kwa kipindi fulani,” imeeleza.

Taarifa hiyo imesema uchunguzi wa awali umebaini kampuni ya LBL imekuwa ikikusanya fedha kwa kutumia mtandao kutoka kwa wananchi pasipo kufuata taratibu zozote za kisheria.

Send this to a friend