Trump amfuta kazi kiongozi mkuu wa kijeshi Marekani

0
6

Rais Donald Trump amemfuta kazi Jenerali wa Jeshi la Anga ambaye ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Majeshi wa Marekani, Jenerali Charles Q. Brown na kumteua Luteni Jenerali wa Jeshi la Anga, John Dan “Razin” Caine, ambaye tayari amestaafu.

Jenerali Brown alikuwa afisa wa pili mweusi katika historia ya Marekani kushikilia nafasi hiyo ya juu, ambayo inatoa ushauri kwa Rais na Waziri wa Ulinzi kuhusu masuala ya usalama wa taifa.

Dakika chache baadaye, Waziri wa Ulinzi, Pete Hegseth  ametangaza kumfuta kazi mkuu wa jeshi la wanamaji, Admiral Lisa Franchetti, mwanamke wa kwanza kuhudumu katika Wakuu wa Majeshi.

Waziri wa Ulinzi Pete Hegseth hapo awali alisema kwamba Jenerali Brown alipaswa kufutwa kazi kwa sababu ya msimamo wake unaolenga utofauti, usawa, na ujumuishaji katika jeshi, unaotajwa kuwa unaleta changamoto kwa mfumo wa kijeshi.

Trump alionyesha kutokuwa na imani na viongozi hawa, akisema kwamba mabadiliko hayo yalikuwa sehemu ya juhudi za kuweka viongozi wapya ambao wangeweza kuzingatia majukumu ya kijeshi muhimu ya kuzuia, kupigana na kushinda vita..

Send this to a friend