
Watu ishirini na tano wamelazwa hospitalini baada ya kula nyama ya ng’ombe aliyekufa katika eneo la Masindoni, Chepalungu, Kaunti ya Bomet nchini Kenya.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Bomet, Edward Imbwaga, waathiriwa ni watoto na watu wazima waliokula nyama ya ng’ombe ambaye alikuwa mgonjwa kwa takriban wiki mbili na hatimaye kufa.
Polisi wamsaka mwanamke kwa tuhuma za kumuua mchepuko wa mume wake
Taarifa ya Polisi imesema kuwa waliokula nyama hiyo walipatwa na kuharisha, kichefuchefu na kutapika mara baada ya kula. Kutokana na hali hiyo, mkuu wa eneo hilo, Richard Koech na uongozi wa nyumba kumi, waliwasaidia waathiriwa kupelekwa hospitalini.
Baada ya tukio hilo, mmiliki wa ng’ombe huyo, Janeth Terer, mwenye umri wa miaka 39, alikamatwa kwa kuruhusu nyama hiyo kusambazwa kwa wanakijiji ambapo amewaeleza polisi kuwa hakuna mtu wa familia yake aliyekula nyama hiyo.