Zaidi ya wanamgambo 70 wa Al- Shabaab wauawa Somalia

0
19

Serikali ya Somalia imesema zaidi ya wanamgambo 70 wa kundi la Al-Shabaab wameuawa nchini humo katika operesheni ya jeshi kwa ushirikiano na vikosi vya ndani.

 Mbali na kuwaua wanamgambo hao, jeshi pia limekamata silaha nyingi na kuharibu magari kadhaa ya vita yaliyokuwa yakitumiwa na wanamgambo hao.

Operesheni hiyo ilifanyika Jumanne katika maeneo mbalimbali ya jimbo la Hirshabelle, kusini mwa Somalia.

“Magaidi wa Al Shabab walishindwa vibaya,” amesema mkazi mmoja wa jimbo hilo akiongeza kuwa miili ya wanamgambo hao ilionekana kwa wingi katika maeneo ya mapambano.

Kundi la Al Shabab, linalohusiana na Al Qaeda, limekuwa likipambana na serikali ya Somalia kwa zaidi ya miaka 15 likitaka kutekeleza sheria zake nchini humo.

Send this to a friend