Zelensky kukutana na Trump kusaini makubaliano ya madini

0
3

Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky atakutana na Rais wa Marekani, Donald Trump mjini Washington siku ya Ijumaa kusaini makubaliano yatakayoiruhusu Marekani kupata rasilimali za madini adimu nchini Ukraine.

Trump amesema makubaliano hayo yatasaidia walipa kodi wa Marekani kufidia fedha zao zilizotolewa kama msaada kwa Ukraine wakati wa vita na Urusi.

“Tumeweza kufikia makubaliano ambapo tutapata pesa zetu tena, na tutapata pesa nyingi zaidi siku zijazo,” Trump alisema katika mkutano na Baraza lake la Mawaziri.

Kyiv inakadiria kuwa takriban asilimia 5 ya malighafi muhimu duniani zipo Ukraine. Nchi hiyo pia ina akiba kubwa ya madini adimu yanayotumika kutengeneza silaha, mitambo ya upepo na vifaa vya kielektroniki.

Zelensky amesema anatumaini kuwa makubaliano hayo ya awali na Marekani yatafungua milango kwa mikataba zaidi.

Send this to a friend