
Uchunguzi wa ndani wa Jeshi la Israel kuhusu shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023, umekiri kuwa jeshi lilishindwa kabisa kuzuia shambulio hilo na kushindwa kuwalinda raia, likisema kwa miaka mingi lilidharau kundi hilo.
Shambulio hilo liliua mamia ya Waisraeli na kusababisha vita vikali huko Gaza, ambavyo vimesababisha vifo vya maelfu ya Wapalestina.
“IDF ilishindwa kuwalinda raia wa Israel. Kitengo cha Gaza kilishindwa mapema kabisa wakati wa shambulio hilo, na magaidi wakachukua udhibiti na kufanya mauaji katika jamii na barabara za eneo hilo,” imesema ripoti hiyo.
Uchunguzi huo unahusisha ripoti 77 tofauti kuhusu matukio yaliyojitokeza katika jamii, kambi za jeshi, na maeneo mbalimbali ya mapambano karibu na mpaka wa Gaza.