Jay-Z amfungulia kesi mwanamke aliyemtuhumu kwa ubakaji

0
5

Mwanamuziki Jay-Z amemshitaki mwanamke aliyefuta kesi aliyomtuhumu kwa ubakaji baada ya tuzo za MTV Video Music Awards za mwaka 2000 akiwa na umri wa miaka 13.

Kesi ya Jay-Z, iliyowasilishwa katika mahakama ya shirikisho huko Alabama, pia inamshtaki wakili wa mwanamke huyo, Tony Buzbee, na wakili mwenzake, David Fortney, kwa kuandaa kesi hiyo. Hata hivyo, Buzbee amekana kufanya makosa yoyote na anadai timu ya Jay-Z ilimtisha mwanamke huyo ili abatilishe taarifa zake.

Mwanamke huyo ambaye jina lake halijajulikana, alikiri kwa hiari kuwa alishinikizwa kutoa madai ya uongo ili kujipatia pesa.

Jay- Z amesema shutuma hizo zimesababisha madhara kwake binafsi na kazi yake, ikiwa ni pamoja na kupoteza kandarasi za biashara zenye thamani ya takriban dola za kimarekani milioni 20 [bilioni 52.2] kwa mwaka katika kampuni yake, Roc Nation, na kuiathiri familia yake, hasa watoto wake.