Wateja wa Benki ya Exim Kufurahia Huduma za Kipekee Kutoka CIP Lounge katika Uwanja wa JNIA

0
2

Benki ya Exim Tanzania imetangaza ushirikiano wa kimkakati na CIP Lounge iliyopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Terminal 3, Dar es Salaam, ili kuwapa wateja wake huduma za kipekee za mapumziko kabla ya kuanza safari zao. Ushirikiano huo unaonesha dhamira ya benki hiyo katika kuboresha maisha na urahisi wa wateja wake kwa kuwapatia faida maalum zinazozidi huduma za kawaida za kibenki.

Kupitia ushirikiano huu, wateja wa daraja la juu wa Benki ya Exim watapata huduma za CIP Lounge bila malipo, wakihakikishiwa utulivu na faraja kabla ya safari zao. Aidha, wateja wote wengine wanaotumia kadi za benki hiyo watapata punguzo la 30% kwenye manunuzi yanayofanywa ndani ya CIP Lounge, na hivyo kufurahia safari yao.

AkizungumzIa ushirikiano huo, Bw. Shani Kinswaga, Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya Exim, amesisitiza dhamira ya benki hiyo ya kuwapatia wateja wake thamani ya ziada: “Sisi kama benki ya Exim, tunatafuta njia bunifu za kuboresha huduma kwa wateja wetu zaidi ya huduma za kifedha. Ushirikiano huu na CIP Lounge katika Uwanja wa Ndege wa JNIA ni uthibitisho wa dhamira yetu ya kuwapatia wateja wetu urahisi, uharaka, faraja, na huduma za kifahari. Iwe wanasafiri kwa ajili ya biashara au mapumziko, wateja wetu sasa wanaweza kufurahia huduma bora katika uwanja huo, na hivyo kufanya safari zao kuwa bora na za kufurahisha zaidi.”

Ofisa Mkuu wa Fedha kutoka benki ya Exim, Shani Kinswaga (kushoto) na Mkurugenzi wa kampuni ya Dough Works Limited, waendeshaji wa CIP Lounge, Vikram Desai wakisaini nyaraka za makubaliano kwa lengo wateja wao kufaidika na ofa mbalimbali za CIP Lounge iliyopo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) katika tukio lililofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 5 Machi 2025.

Naye Stanley Kafu, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki ya Exim, aliongeza: “Wateja wetu wa daraja la juu sasa wanaweza kufurahia huduma za CIP Lounge bila gharama yoyote, wakipata mazingira tulivu na yenye hadhi ya juu ya kupumzika kabla ya safari zao. CIP Lounge inatoa sehemu ya kupumzikia mbali na msongamano wa abiria, ikiwawezesha wasafiri kupata utulivu au kufanya kazi zao kwa faraja.”

Stanley aliongeza kuwa, “Kwa wateja wa benki yetu wasio na huduma ya bure pale CIP Lounge, tunajivunia kuwapatia punguzo la 30% kwenye manunuzi yote yanayofanyika ndani hapo. Hii inahakikisha kuwa wateja wengi zaidi wanapata fursa ya kufurahia huduma hizi za hali ya juu kwa gharama nafuu, na kufanya safari zao kuwa za kuvutia zaidi.”

“Tunapenda  kila wakati kuvumbua mbinu za kuwapatia wateja wetu manufaa yanayozidi huduma za kawaida za benki, tukidumisha dhamira yetu ya kuboresha maisha ya wateja wetu. Mpango huu unaendana na mkakati wetu wa kujenga uhusiano wa karibu na wateja kwa kuunganisha huduma za kifahari na za kifedha,” alihitimisha Stanley.

CIP Lounge inajulikana kwa mandhari yake ya kifahari, ikiwaruhusu wasafiri kupata sehemu tulivu ya kupumzika mbali na pilikapilika za uwanja wa ndege. Wageni wanaweza kufurahia mlo bora wa hali ya juu, vinywaji vya daraja la kwanza, na sehemu ya nje yenye mandhari nzuri, yote yakilenga kutoa huduma za kipekee kabla ya safari.

Mkurugenzi wa Dough Works Limited, ambao ni waendeshaji wa CIP Lounge, Vikram Desai, alielezea furaha yake kwa ushirikiano huu: “Tunayo furaha kushirikiana na benki ya Exim kuwapatia wateja wao huduma bora za kiwango cha juu. Katika CIP Lounge, tunajivunia kutoa huduma za kipekee za ukarimu, zenye faraja ya hali ya juu, huduma binafsi, na mazingira mazuri yanayowawezesha wasafiri kupumzika, kufanya kazi, au kupata utulivu kabla ya safari zao.

Ushirikiano huu unaendana kikamilifu na dhamira yetu ya kuboresha huduma za mapumziko kwenye viwanja vya ndege na kuwapatia abiria utulivu wa kusafiri ulioimarishwa.”

Kwa kuwapatia wateja wake huduma za kifahari katika viwanja vya ndege, benki hiyo inaendelea kuinua kiwango cha kuridhika kwa wateja na kupanua ahadi yake ya kuwapatia urahisi zaidi ya huduma za kawaida za kibenki. Iwe wateja wanahitaji kupumzika, kufurahia mlo wa hali ya juu, au kupata sehemu ya kipekee kabla ya safari, ushirikiano huu unahakikisha wanapata faraja na huduma za hali ya juu wanazostahili.

Kadri benki ya Exim inavyoendelea kutoa suluhisho bunifu zinazokidhi mahitaji ya maisha ya kisasa, mpango huu unathibitisha tena ahadi yake ya kuwapatia wateja thamani katika kila hatua ya safari zao. Iwe ni safari za kibiashara au burudani, wateja wa Exim sasa wanaweza kufurahia safari zisizo na usumbufu—ikiwa ni kielelezo cha dhamira ya benki hiyo ya kutoa huduma za kibenki za kiwango cha kimataifa zenye manufaa ya ziada.